Powered By Blogger

Kuna umuhimu wa kufanya mazoezi?

Tuesday, January 31, 2012

FAIDA UNAZOPATA UKIFANYA MAZOEZI MBALIMBALI YA AEROBICS KWA MUDA WA WIKI NNE BILA KUACHA



FAIDA UNAZOPATA KUTOKANA NA MAZOEZI YA AEROBICS

-Kukuongezea uwezo wa kupumua kwa ufasaha na uhakika.

-Kuuweka moyo wako kuwa madhubuti katika msukumo wa damu mwilini.

-Kupunguza mapigo ya moyo ambayo si ya kawaida.

-Kuongeza uwezo wa mzunguko wa damu na kuchuja mafuta kwenye damu kwa

uhakika zaidi.

-Kusaidia kupunguza mafuta kwenye mwili kwa kiasi kikubwa.

-Kusaidia kupunguza uzito ulokithiri.

-Kuongeza mtiririko wa hewa ya oksijeni kwenye damu.

-Kuufanya mwili kuwa na uwezo wa kulainisha misuli ya mwili.

-Kukukinga na maradhi ya mara kwa mara na kuongeza seli nyekundu za mwili.

KWA MASWALI ZAIDI KUHUSU MAZOEZI NIANDIKIE KUPITIA

omaryswai@gmail.com

Thursday, January 26, 2012

WAALIMU WA AEROBICS WAMALIZA KOZI YA AWALI KWA KUFANYA MTIHANI CHUO KIKUU CHA MLIMANI (UDSM PESS)

Katika chuo kikuu cha Mlimani Shule ya Elimu ya Juu,kitengo cha Sayansi mazoezi ya viungo na michezo imemaliza kozi ya awali ya waalimu wa aerobics na gym hivi karibuni kwa kufanya mtihani wa natharia na vitendo.
















Katika picha ya pamoja wanafunzi waliomaliza
kozi ya awali ya aerobics na gym wakiwa na
mwalimu wa aerobics O.Swai aliyevaa kofia
nyekundu.















Hapa ni baadhi ya wanafunzi wakifanya mtihani
wa vitendo wakisimamiwa na mkuu wa kitengo cha
cha PESS Dk. C.Maro ambaye ameshika kitabu
katika picha kati.

Tuesday, January 24, 2012

MAZOEZI YA KICKBOXING KATIKA AEROBICS

Katika mzoezi ya viungo huwa kuna aina nyingi za mazoezi ambayo haya yote hugusa hisia na sehemu mbalimbali za misuli ya mwili wa binaadamu.
Mazoezi hayo ambayo hufanywa kwa kufuata muziki ambao ni maalumu kwa zoezi hilo, yakiwemo mazoezi ya kickbox unafanya kwa kufuatilia muzuki na pindi ufanyapo utasikia kamavile unapigana lakini sivyo ni aina ya mazoezi ya viungo, na pindi umalizapo unasikia akili na mwili wako kweli umefanya zoezi tosha.



















Katika picha hapo juu mwalimu Swai akifundisha
mazoezi ya kickbox ambayo yamependwa sana
na wadau wa aerobics


















Master class Omar swai akiuonyesha mdau wa
aerobics namna ya kutupa ngumi na teke kwa
pamoja.

Wednesday, January 11, 2012

UMUHIMU WA MAZOEZI YA TUMBO

Mara nyingi watu watu huona mazoezi ya tumbo huwa ni magumu sana kwa mtu anayefanya, lakini yana umuhimu wake mkubwa katika maisha ya kila siku.

Umuhimu wa kufanya mazoezi ya tumbo iwe kwa mwanamke au mwanaume unatakikana hii ni kwa ajili ya kuuweka mwili wako katika hali ya kupendeza pindi ukiwa umevaa nguo zako kuweza kukuenea na kuonekana nadhifu na kupendeza.
Hivyo mazoezi ya tumbo pia hukufanya kukazika kwa misuli ya tumbo na kuwa unatembea umenyooka na kuvutia.
















Hapa mwalmu henry akiwa anafanya mazoezi
ya tumbo kwa staili mbali mbali.

Tuesday, January 3, 2012

MAZOEZI YA KUONDOA TUMBO

NAMNA YA KUFANYA MAZOEZI YA TUMBO

Katika picha (a)1 inaonyesha namna ya kuanza kufanya mazoezi ya tumbo na maelezo yake.
Unalala chali kuhakikisha mgongo wako umekandamiza chini kabisa na mikono yako yote miwili ikiwa nyuma ya shingo yako na viwiko vyako vikiwa umenyoosha pande zote, halafu unavuta pumzi ndani kwa kutumia pua kabla ya kunyanyuka


Picha(a)1















Katika picha (b)1 unanyanyuka juu kwa
kunyanyua sehemu ya mabega yako yote
wakati huo unahakikisha unakaza misuli
yatumbo lako pindi unapokuja juu na hapo
ndipo unatoa pumzi kwa kupitia mdomoni
mwako ukiwa una fikia juu na kurudi chini
tena nakuanza kama picha (a)1 invyoonyesha
mara kumi .
unafanya seti 5x10

Picha (b)1






















Zoezi la pili la tumbo picha (a)2 inaonyesha
namna ya kuanza hilo zoezi.
Unakunja muguu yako yote miwili huku
umeweka mikono yako nyuma kwa ajili
ya kujizuia usende nyuma zaidi na kubalasi
mwili wako wakati wa zoezi lenyewe.


Picha(a)2


















Halafu unanyoosha miguu yako kabla ya kufikia kunyooka
unarudia tena kukunja kama picha (a)2 inavyoonyesha.
Kwa kufanya hivyo unatakiwa ufanye mara kumi seti tano
5x10 baada ya hapo unapumzika kwa dakika moja na kurudi
tena.
Usisahau kuvuta pumzi ndani pindi ukunjuapo na kupumua nje
unyooshapo miguu yako.


Picha (b)2