Mwalimu Dulla ameonekana kuwa nyota na hii ni bidii pamoja na ubunifu wake katika mazoezi ya aerobics katika nchi za ughaibuni hivi karibuni.
Hii ilidhihirisha tangu alipokuwa Dubai na kufundisha mashirika mbali mbali moja wapo ni shirika la ndege la huko Dubai kwa kuwafundisha marubani na wahudumu wake.
Kutokana na umashuhuri wake na uelewa wa kufundisha mambo ya aerobics hivi sasa anafundisha katika chuo kimoja cha kijeshi huko Abudhabi.
Hii ni kutokana na bidii ya kujielimisha zaidi katika fani hii ya mazoezi.
Katika picha hapo chini mwalimu Dula akiwa anafundisha wafanyakazi wa shirika la ndege huko Dubai
No comments:
Post a Comment