Powered By Blogger

Kuna umuhimu wa kufanya mazoezi?

Wednesday, February 23, 2011

WANAFUNZI WA CHUO KIKUU PESS WAITEMBELEA GYM YA TANZANED

Hii ikiwa ni mara ya kwanza kwa wanafunzi wa chuo kikuu kutembelea gym za mazoezi ili nao waone jinsi wenzao wanavyoendesha gym na kuona pia mambo yale walosomea yanaenda vipi,na hii inaleta changamoto pindi wamalizapo chuo na kuajiriwa katika sehemu za mazoezi za watu binafsi au vyuo.



Katika picha inaonyesha wanafunzi wakiwa kwenye darasa la spinner.Mbele waliosimama kulia ni mkuu wa kitengo cha michezo na sayansi Dr.Maro kushoto ni mwalimu O.Swai mkuu wa msafara na mwalimu wa aerobics chuoni hapo.












Mazoezi ya tumbo





Mwalimu Fracis wa gym ya Tanzaned akiwaonyesha wanafunzi wa chuo kikuu namna ya kufanya mazoezi ya tumbo kwa kutumia mipira maalum








Hapa mwalimu Francis akimuelekeza mwanafunzi wa chuo kuu udsm mazoezi ya tumbo kwa kutumia mashine

Saturday, February 19, 2011

WANAFUNZI WA CHUO KIKUU (PESS) WATEMBELEA GYM YA GENESSIS

Katika mafunzo ambayo wanayopata wanafunzi wa chuo kikuu Pess ni pia moja wapo ya ujasiriamali pindi watokapo hapo chuo ili waweze kumudu maisha yao wakiwa uraiani iwe ni kujiajiri au kuajiriwa katika soko la gym.
Pamoja na kuwa na gym ya mazoezi hapo chuoni pia hutembelea gym nyingine na kuona zinavyoendeshwa kwa maandalizi ya wao kuajiriwa wamalizapo mafunzo ya gym na aerobics



Katika picha ya pamoja Mwalimu Swai akiwa na wanafunzi wa chuo walipotembelea Genessis gym.








Katika picha za chini zinaonyesha Mwalimu Sas akitoa maelelozo kwa wanafunzi wa chuo kikuu mlimani PESS baadhi ya mashine na matumizi yake hapo katika gym ya Genessis

Saturday, February 12, 2011

MWALIMU DULLA AKIWA HUKO DUBAI NA WAALIMU WENZAKE

Mwalimu Dulla akiwa kwenye picha ya pamoja na waalimu wenzake huko Dubai picha ya juu. halikadhalika chini kwenye picha ya pamoja na wanafunzi wake anaofanyisha mazoezi ambao ni wafanyakazi wa Etihed air ni pamoja na wahudumu wa ndege na marubani amevaa kofia kasimama nyuma wa tatu toka kushoto.


Wednesday, February 2, 2011

MWALIMU DULLA APANDA CHATI YA UFINDISHAJI BORA WA AEROBICS DUBAI

Mwalimu Dulla ameonekana kuwa nyota na hii ni bidii pamoja na ubunifu wake katika mazoezi ya aerobics katika nchi za ughaibuni hivi karibuni.
Hii ilidhihirisha tangu alipokuwa Dubai na kufundisha mashirika mbali mbali moja wapo ni shirika la ndege la huko Dubai kwa kuwafundisha marubani na wahudumu wake.

Kutokana na umashuhuri wake na uelewa wa kufundisha mambo ya aerobics hivi sasa anafundisha katika chuo kimoja cha kijeshi huko Abudhabi.
Hii ni kutokana na bidii ya kujielimisha zaidi katika fani hii ya mazoezi.


Katika picha hapo chini mwalimu Dula akiwa anafundisha wafanyakazi wa shirika la ndege huko Dubai