Mara nyingi kipindi hiki cha mwezi wa Desemba wadau wengi wa mazoezi huwa ni wakati wa kupumzika na kukaa na familia zao, ambao kwa muda mrefu watoto wao walikuwa mashuleni.
Hata hivyo wengine ni wakati muafaka kwa wao kuchukua likizo na kusafiri kuelekea makwao.
Kwa makusudi ninazungumzia kipindi cha skukuu ya krismas ambacho mtu huenda kula bila ya mpangilio na hata kusababisha maradhi ambayo hapo awali aliweza kuyamudu kwa kufanya mazoezi.
Jambo la muhimu ni kujaribu kuchunga usirudi pale ulikotoka na kujiweka katika afya madhubuti uliyonayo hapo mwanzoni kipindi ufanyapo mazoezi.
Kuwe na umuhimu wa kujichunga na uzito ulokithiri kwa kufuata mpangilio wako wa kila siku. Yaani usizidishe chakula kupita ili kuchunga kuongezeka uzito usio na mpangilio maana baada ya siku unaanza palepale kama zamani.
Nini cha kufanya ni wewe kujaribu kutokula wanga kwa wingi na wakati wa usiku upate chakula chepesi.
Nakutakieni KRISMASI NJEMA NA AFYA NJEMA.
No comments:
Post a Comment