Powered By Blogger

Kuna umuhimu wa kufanya mazoezi?

Saturday, September 25, 2010

MWALIMU YASINI AKIWA KATIKA DARASA LA MAZOEZI YA TUMBO KATIKA GYM YA TANZANED

Mwalimu Yasini ni mwalimu aliye makini katika kufundisha mazoezi yaviungo, akiwa amebobea kwa muda mrefu. Wadau wa mazoezi ya viungo wamefaidika naye kujaribu kuwasaidia kuondoa matatizo ya uzito akiwa katika gym ya Tanzaned na gym nyingine anazofundisha jijini Dar es salaam.

Katika picha mwalimu Yasin akitoa maelekezo nakuangalia kama wadau wanafanya vyema mazoezi mbalimbali ya tumbo.







Thursday, September 23, 2010

MWALIMU FRANCIS KATIKA DARASA LA SPINNER

Mazoezi ya spinner yametokea kupendwa na wadau wengi wa mazoezi japo siyo siku nyingi kuanzia hapa bongo.
Mwalimu Francis ni mmoja wa waalimu anayefundisha mazoezi ya spinner katika gym ya Gymkhana club ya Dar es salaam




MWALIMU FRANCIS akiwa kwenye darasa lake la spinner (baiskeli za mazoezi)


















Wadau wa mazoezi wakifuatilia kwa makini master class O.Swai nae alikuwepo.













Monday, September 20, 2010

BONANZA LA AEROBICS PAMOJA NA FAMILIA

Aquar Aerobics vilevile ilikuwepo ili mradi kupata burudani isiyo kifani pamoja na familia katika hoteli ya South beach iliyopo Kigamboni.
AQUA AEROBICS


























Pamoja na michezo mingine hapa ni volleyball
Ni muhimu kuchanganya mazoezi ili usichukie mazoezi na kukutana na familia.

BONANZA LA AEROBICS PAMOJA NA FAMILIA

Ni katika burudani na pata shika nguo kuchanika baada ya aerobics pia kuna michezo mingine kama voleyball na familia kupa msosi.
Pamoja na kupongezana kwa zawadi






Saturday, September 18, 2010

MAZOEZI YA AEROBICS NI KWA AJILI YANINI

MAZOEZI YA AEROBICS NI KWA AJILI YA NINI
Mazoezi ya aerobics ni kwa ajili kila mtu bila kujali jiinsia au umri hii ni kwa ajili ya watu wote ambao wameamua kufanya mazoezi ya mwili kwa ajili ya afya zao.

Baada ya utafiti wangu wa takriban miaka kumi katika mazoezi ya aerobics, darasa la aerobics lilikuwa likihudhuriwa na idadi kubwa ya wanawake kuliko wanaume hii ilikuwa ni fikra potefu walizokuwa nazo wanaume kwamba mazoezi ya aerobics ni kwa ajili ya wanawake tu.

Lakini kuanzia mwaka wa 2000 kumekuwa na mabadiliko kwa wanaume wengi kujiunga na mzoezi ya aerobics hivi sasa kuna mwamko mkubwa kwa wanaume kufanya haya mazoezi. Katika kufanya mazoezi aerobics inaupa mwili uwezo wa kupitisha hewa ya oksijen kwa urahisi zaidi na uhakika na pia kuupa moya uwezo wa kupiga mapigo yake kwa dakika wakati unapofanya mazoezi.

Mazoezi ya aerobics ni lazima yafanyike japo kwa muda wa dakika 30-60 na iwe ni mara 3 au 5 kwa wiki kwa ajili ya kuufanya mwili kuwa mchangamfu kwa wakati wote na kupunguza mafuta na uzito uliokithiri.

Thursday, September 16, 2010

FAIDA ZA KUFANYA MAZOEZI KATIKA MAISHA YAKO

JE UNAJUA KILA MARA UFANYAPO MAZOEZI UNAFAIDIKA VYEMA NA AFYA YAKO

ZIFUATAZO NI SIRI ZA MAFANIKIO YA MAZOEZI

1.MAZOEZI HUSAIDIA KATIKA MFUMO WA USAGAJI CHAKULA KUWA MZURI NA UHAKIKA NA KUPELEKA SEHEMU INYOHUSIKA KWA MUDA MUAFAKA.

2.MAZOEZI HUKUFANYA KUJISIKIA NA AFYA NJEMA KUKUPA NGUVU NA KUWEZA KUFANYA KAZI KWA NGUVU ZAKO BILA KUJISKIA UMECHOKA NA MWISHO WA SIKU HUPUNGUZA MAFUTA MWILINI.

3.MAZOEZI HUPUNGUZA UZITO, KUNYOOSHA NA KUIMARISHA MISULI YA MWILI.

4.KUPUNGUZA PRESHA.

5.HUSAIDIA KUPUNGUZA MAFUTA

6. HUONGEZA HDL VIZURI.

7. HUSAIDIA MAPIGO MAZURI YA MOYO KWA KUONGEZA KASI YA MAPIGO YAKE WAKATI WA MAZOEZI.

8. HUONGEZA CHEMBE CHEMBE YEKUNDU KWENYE MZUNGUKO WA DAMU AMBAZO ZINABEBA OKSIJEN KWENYE MAPAFU NA PELEKA SEHEMU NYINGINE ZA MWILI.

9.UNGUZA MRUNDIKO WA DAMU KWENYE MISHIPA, HII NI MUHIMU KWA SABABU MGANDO WA DAMU HUSABABISHA MAGONJWA YA MOYO PAMOJA NA KUPOTEZA FAHAMU.

10.MAZOEZI HUIMARISHA MIFUPA YA MWILI

11.HUSAIDIA KUPANUA MISHIPA YA DAMU INAYOPELEKA KWENYE MOYO

12HUSAIDIA KUFANYA MISULI YA MOYO KUWA MADHUBUTI.

13.HUPUNGUZA KIASI CHA MAFUTA YALIKO KWENYE DAMU.

14.MAZOEZI HUSAIDIA KUPUNGUZA UGONJWA WA KISUKARI.

15.HUBORESHA USINGIZI.

16.HUSAIDIA MMOMONYOKO WA CHAKULA AMBAO HUSAIDIA KUPUNGUZA MAGONJWA YA KANSA.

17.MAZOEZI HUSAIDIA KUIMARISHA SEHEMU ZA VIUNGO VYA MWILI.

18.MAZOEZI HUSAIDIA MAAMBUKIZO YA INDOMETRIOSIS KWA ASILIMIA 50% KWA WANAWAKE.

19.MAZOEZI HUONGEZA KIASI CHA DAMU AMBACHO HUSAMBAA NA KUIFANYA NGOZI KUONEKANA YENYE AFYA ZAIDI

20.MAZOEZI HUKUFAYA UJISIKIE MCHANGAMFU
NA AFYA.

MAZOEZI YA VIUNGO NA SARAKASI GYMNASTIC

Watu wengi hufikiria vijana wanaofanya mchezo huu wa sarakasi huwa wanatumia mazingaumbwe, hapana ni kutokana na mazoezi ya kila siku ya viungo katikamaisha yako hii hukusaidia kuwa mwepesi na kuwa na balasi ya mwili wako.


KATIKA PICHA VIJANA WAKIFANYA VITU VYAO KUWABURUDISHA WATU.

Wednesday, September 15, 2010

JE UMEFIKA BIGGY RESPECT VAA UPENDEZE

KARIBU KATIKA DUKA LA BIGGY RESPECT KWA KUNUNUA NGUO
VIATU HATA NA JEZI PAMOJA NA NGUO ZA MAZOEZI.

BROTHER MUSSA KISSOKY AKIJIFUA KATIKA GYM YA KILIMANJARO

Mussa Kissoki ni mkurugenzi wa Sofia Records ambae ni mdau wa siku nyingi katika mazoezi hapa akifanya mazoezi ya kujenga kifua.


RED'S GYM KATIKA KUFUNDISHA NGUMI ZA KULIPWA

KIJANA AMBAE ANACHIPUKIA KATIKA FANI YA NGUMI ZA KULIPWA KWENYE GYM YA RED'S INAYOMILIKIWA NA FIKE AMBAYE ALIKUWA MR.TANZANIA GINESS MIAKA YA MWISHO YA 98 ILIYO KOKINODONI
AKIFANYA MAZOEZI KATIKA PUCHI BEGI KAMA PICHA ZINAVYOONYESHA.