Mara nyingi watu hudhani kuwa kufanya dayati ni kutokula kabisa, la hasha hizo ni fikra potofu kwa mwana mazoezi ambazo zimerithiwa na wale ambao hawajui namna au maana ya dayati, Dayati maana yake ni kubadili mfumo wako wa kula kula bila ya mpangilio.
Kubadilisha tabia ya kula bila mpangilio na kula kiasi kidogo cha chakula haswa wakati wa usiku ili kuepuka uzito maana nyakati za usiku unakuwa hufanyi shughuli yoyote ile ya kutumia chakula ambacho ulichokula kwa usiku ule hivyo basi kile chakula hubadililika na kuwa mafuta na kwenda kujikusanya sehemu mbalimbali ya mwili wako. Kwa wale ambao hawafanyi mazoezi hupata shida ya kuongezeka uzito mara kwa mara.Kama unataka kupungua uzito punguza chakula unachokula na kula mboga za majani kwa wingi na mtunda kwa ajiliya kuepuka vyakula venye mafuta mengi. Fanya mazoezi japo mara tatu kwa wiki.
MAZOEZI AINA MBALI MBALI KWA KUJIWEKA NA AFYA NZURI YA MWILI WAKO
Mazoezi ya tumbo kuondoa mfutaZoezi la kunyoosha misuli ya mgongo
Kufanya mazoezi ya Aerobics kwa ajili ya kupunguza uzito
Mazoezi ya kutengeneza misuli yako na kuonekana nadhifu