Wana mazoezi wengi hawazingatii kufanya mazoezi ya kunyoosha mwili(stretching exercise) baada ya kumaliza zoezi husika ipasavyo.
Kwa kufanya mazoezi ya kunyoosha misuli(stretching exercise) husaidia kwa kiasi kikubwa kukuepusha maumivu yamisuli mwilini mwa mwana mazoezi na kusaidia kuirudisha misuli yako kwenye hali yake ya kawaida. Nikimaanisha kuwa pindi ufanyapo mazoezi misuli ya mwili huwa mifupi na kukaza kwa ajili ya kukupa uwezo na nguvu kipindi ufanyapo mazoezi, misuli hutanuka ili kukupa nguvu zaidi. Ili irejee katika hali yake ya kawaidi ni muhimu sana kufanya mazoezi ya kunyoosha misuli(stretching) baada ya mazoezi.
Lakini ukumbuke huwezi nyoosha misuli (stretching) kabla ya kupasha misuli joto(warm up). Hii husaidia kutayarisha misuli yako kwa kuipa joto na kupeleka mapigo ya moyo wako sambamba kwa zoezi lifuatalo, pia kuepuka kuumia kwa misuli wakati wa mazoezi. Kunyoosha mwili (stretching) husaidia kupunguza msongamano wa mawazo.Tafiti zimeonyesha pia husaidia kuondoa ganzi na kuwa mchangamfu wa misuli kwa kufanya mazoezi ya kunyoosha mwili(stretching) kila siku
Wanamazoezi ya Aerobics wakinyoosha mwili(stretching) baada ya zoezi