Powered By Blogger

Kuna umuhimu wa kufanya mazoezi?

Saturday, September 5, 2015

MAMBO MUHIMU AMBAYO MJENGA MISULI YAANI BODY BUILDER ANATAKIWA KUFANYA NA CHAKULA ANACHOTAKIWA KULA.

Kama nilipozungumzia hapo awali kwa wale wapenzi wa kujenga misuli na kuonekana ana misuli mikubwa zaidi.Jambo la muhimu ni kupata miilo ambayo sio chini ya mara tano, hii ikiwa ni pamoja na kupata aina ya chakula cha protini ya kutosha, ambacho husaidia kukuza misuli kwa haraka na uhakika.

Kadhalika kupata aina ya chakula cha wanga ili kuupa mwili nguvu ya kuweza kunyanyua uzuto mkubwa kwa ajili ya kujenga misuli .Pia kupata muda wa kutosha kupumzika kwa ajili ya kuwezesha mwili kukuza misuli kwa matokeo ya mazoezi ya siku ile.

Hakikisha wakati wote tumbo lako lina chakula nikimaanisha kutokuwa na njaa kipindi chote.

Maji ni muhimu katika maisha ya mjenga misuli na pia mtu yeyote yule anayefanya mazoezi/