AINA ZA VYAKULA NA WAKATI MUAFAKA WA KULA
1.Aina ya vyakula vya wanga.
Chakula hiki ni kwa ajili ya kuupa mwili nguvu na mara nyingi hutumika wakati wa mchana kwa sababu unafanya kazi iwe ni ya ofisini au shambani, aina yenyewe ni kama vile ugali wa dona,wali,ugali wa mtama na ngano.
2.Aina ya vyakula vya protini.
Chakula hiki kinasaidia katika kujenga misuli ya mwili ni muhimu sana haswa kutumika kwa wale wanaofanya mazoezi ya kujenga misuli,pia ni vizuri kuliwa wakati wa asubuhi na jioni na aina yenyewe ni nyama ya kuku, mayai ya kuku, maharage na samaki.
Bila kusahau aina ya mbogamboga na matunda yawemo japo kwenye mlo mmoja.