Wako baadhi ya watu ambao wanaona fahari ya kuwa na kitambi tena hujisifu na kusema kama huna kitambi hutopata heshima na kuonekana mchovu yaani huna pesa.
Mimi sikubaliani nao abani nawaonea huruma kwani tayari wameshakuwa ni wagonjwa japo wao hujiona ni afya.
Kuwa na kitambi ni maradhi ambayo unatembea nayo lakini baada ya siku unakuja kugundua kumbe ulikuwa mgojwa, kwa sabababu kuwa na kitambi ni mkusanyiko wa mafuta yaliyokithiri mwilini ambayo hutakiwi kuwa nayo.
Mwanadamu kwa kawaida akizidiwa na mafuta mwilini huwa anakuwa na uwezekano mkubwa wa kupata maradhi ya presha na tena isitoshe ni rahisi pia kupata ugonjwa wa kisukari.
Nawashauri wale wenye vitambi kuondoa mawazo potofu ya kuonekana na kitambi ni heshima, fanya mazoezi kwa ajili ya afya yako, punguza uzito ulokithiri hapo ndipo utafanya mambo yako ya kila siku na kujisikia mwepesi na kuonekana na mvuto hata ukivaa nguo zako.
MAZOEZI YA AEROBICS YANAVYOWANUFAISHA WADAU WA MAZOEZI KATIKA GYM YA UNIVERSITY MLIMANI KATIKA PICHA MBALI MBALI .