Powered By Blogger

Kuna umuhimu wa kufanya mazoezi?

Friday, April 24, 2015

AINA YA VYAKULA UNAVYOTAKIWA KULA NA NYAKATI ILI KUEPUKA ONGEZEKO LA UZITO WA MWILI WAKO



Kwa  bahati nzuri hapa kwetu  Tanzania tumejaaliwa kuwa na vyakula vya kila aina na uwezo wakuvipata kirahisi kwa namna moja au nyingine tunayo.

Mara nyingi  huwa naulizwa ni wakati gani muafaka wa kula vyakula vya wanga na wakati upi kula vyakula aina  ya protini.

*Mwili wa binaadamu unahitaji aina ya vyakula vya wanga kwa nyakati za mchana kwa sababu ya kukupa nguvu kwa shughuli zako za mchana maana katika utendaji kazi huwa matumizi ya nguvu hutumika sana.(kama vile ugali wa muhogo,wali,chapati,makaroni nk.)

Chakula aina ya protini kwa matumizi ya usiku ni muhimu hii ikiwa na maana  vyakula vya aina ya protini sio rahisi kugeuka kuwa mafuta, hii nikimaanisha huenda kiurahisi kwenye mwili bila ya kurundikana kutokana na matumizi yake ni kila wakati mwilini bila ya kutumia nguvu.( kama vile mboga za majani, samaki,kuku,maharage meupe na matunda ya msimu.)

Kumbuka kuepuka kuongezeka uzito jaribu kula vyakula laini nyakati za usiku.(dinner)