Friday, March 20, 2015
NAMNA YA KUFANYA MAZOEZI HATA UKIWA NYUMBANI KWAKO BILA YA KWENDA KITUO CHA MZOEZI( GYM)
Watu wengi wanafikiri kuwa kufanya mazoezi ni lazima uende kituo cha kufanyia mazoezi (gym) au uwanjani, la hasha hakuna ulazima huo bali unaweza pia kufanyia hata ukiwa ndani mwako ili mradi kuwe na nafasi ya mita moja pande zote nne.
NAMNA YA KUANZA NA KUMALIZIA ZOEZI
Unasimama huku miguu yako imepanuka na kuweka mziki wa aina yoyote ile uipendayo wewe na kuanza kucheza muziki huo kwa muda wa dakika 5 halafu unasimama.
Utapumzika kwa sekunde 30 na kurudia hivyo aidha kwa kuruka ruka ili mradi unaongozwa na muziki wako uupendao.
Utaendelea kufanya hivyo hadi umalizapo aina 5 ya muziki utakuwa umeatokwa na jasho sio la kawida hii itakusaidia wewe kupunguza zile kaloriz ambazo zimezidi mwilini mwako.
Baada ya hapo ukae hadi jasho likauke ndipo uendelee kuoga.
Zoezi hili huchukua muda wa dakika25 tu.
Subscribe to:
Posts (Atom)