Tuesday, October 21, 2014
SIRI YA MAFANIKIO YA KUWA MWANA MAZOEZI BORA YA KUJENGA MISULI
Yafuatayo ni namna ya kuepuka makosa ya kawaida wakati ukifanya mazoezi ya kujenga misuli;
1. Usiache wala kupuuzia mazoezi ya kupasha mwili moto(warm up)
Mara nyingi misuli ambayo inapata maumivu makali ni ile ambayo imekosa mazoezi ya kupasha misuli moto(warm up) kuliko yule aliyeanza na mazoezi ya kupasha moto.
Kabla ya kufanya zoezi la kujenga misuli ni muhimu kupasha misuli kwa muda wa dakika tano hadi kumi kama vile kuendesha baiskeli au zoezi la aerobic ili kupandisha joto la mwili na kuwa tayari kwa kunyanyua uzito.
2.Usiharakishe unapofanya mazoezi ya kujenga misuli.
Wakati wa kubeba uzito ni muhimu kutofanya kwa haraka haraka, fanya pole pole kunyanyua uzito usiwe na haraka kwani kufanya mazoezi tartibu husaidia kujenga msuli husika kwa uhakika zaidi na kuusikia.
3.Epuka kufanya zoezi likazidi kipimo cha uwezo wako.
Wanamazoezi wajenga misuli hufanya zoezi aina moja ka muda mrefu na kufanya kujisikia zoezi hilo linachosha hii sio sahihi, Fanya mazoezi ya kujenga misuli kwa mzunguko unaotakiwa.
4.Usipuuze maumivu ya misuli pindi uyasikiapo jichunguze.
Kama utasikia maumivu makali wakati unafanya mazoezi ya kujenga misuli, unashauriwa kupumzika siku hiyo au kupunguza uzito unaobebe.
5.Usifanye mazoezi ya kujenga misuli bila ya kuvaa viatu vya mazoezi
Viatu husaidia sana kuepuka kuteleza wakati ukiwa unafanya mazoezi ya kunyanyua uzito,ni muhimu sana kuvaa.
Subscribe to:
Posts (Atom)