Powered By Blogger

Kuna umuhimu wa kufanya mazoezi?

Monday, July 15, 2013

NAMNA YA KWENDA NA DAYATI KATIKA MWEZI MTUKUFU WA RAMADHANI

Awali ya yote nawatkia mfungo mwema kwenye mwezi huu mtukufu wa ramadhani wale waislamu popote walipo.
Kuna maswali ambayo mtu unaweza kujiuliza katika mambo yanayohusu ulaji wa mwezi huu mtukufu wa ramadhani ewe mwanamazoezi na namna gani utafanya mazoezi ukiwa  umefunga.
Je utaweza kufanya mazoezi huku umefunga.
Je kuhusu aina gani ya chakula unatakiwa kula.
Katika mwezi huu wa mfungo mtu huwa unachoka ule mda wa jioni ambao unatakiwa kufanya mazoezi inakuwa ni vigumu maana unasikia njaa, kwa hiyo hata mazoezi huwezi kuenda.
Nakupa usauri  wangu katika ulaji wako uchunge sana vitu vya mafuta mengi.
Ukisha maliza kufuturu unywe maji ya kutosha na upunguze kiasi cha chakula ambacho hukuongezea uzito kwa urahisi.
Baada ya kula futari  utembee kwa muda wa dakika 20 baada ya hapo uendelee na mambo yako mengine, hii itakusaidia kusaga kile chakula na kukufanya kuwa mchangamfu.
Upate kahawa baada ya kupata futari hii pia itakusaidia kuondoa yale mafuta yaliyobaki kwenye mishipa yako ya mwili na kuifanya ipanuke na pia huondoa shibe.
Huu ni baadhi ya ushauri kwa wadau wa mazoezi ni muhimu kuzingatia.