Klabu ya mazoezi ya viungo ya VETA chuo cha ufundi stadi Dar es salaam ikiwa imewakaribisha wanamazoezi wenzao kutoka klabu ya Mbagala Joging ikiongozwa na mwalimu wao Adam Gwao ambaye pia ni muasisi wa club hiyo. Mazoezi hayo yalifana sana ambayo yalianza majira ya saa 12 hadi saa moja asubuhi yakiwa yamehudhuriwa na wakuu wa chuo hicho cha Veta.
akiwa mbele ya wanamazoezi na mwalimu Adam Gwao tayari kuanza zoezi la Aerobics
Mazoezi yameanza pamoja na mkuu wa chuo cha Veta (mwenye fulana ya bluu ) akiwa
mstari wa mbele.
Zoezi lilipamba moto kila mtu akiwa mwenye furaha asubuhi hiyo ya mazoezi
Kila mtu alikuwa na usongo wa kufanya zoezi siku hiyo bila kushindwa au kuchoka
Mkuu wa chuo cha Veta Mr. Samwel Ng'andu akizungumza na wanamazoezi
na kuwakaribisha wanamazoezi wa Mbagala club wote wakimsikiliza kwa makini.
Mwalimu O.Swai akitoa mafunzo ya lishe bora baada ya kumaliza mazoezi ya siku hiyo
Akisema "Kufanya mazoezi peke yake hayasaidi ila ni pamoja na kujaribu kubadili tabia
ya kula mlo".