Powered By Blogger

Kuna umuhimu wa kufanya mazoezi?

Saturday, January 29, 2011

MWALIMU DULA AKIWA KWENYE DARASA LA KICK BOXING ABUDHABI

Mwalimu Dulla mwenye jezi nyekundu na kitambaa kichwani akiwa katika moja ya darasa la kick boxing huko ughaibuni Abudhabi

KUANGALIA MAZOEZI YA AEROBICS BONYEZA HAPA

Friday, January 28, 2011

WANAFUNZI WA CHUO KIKUU CHA MLIMANI PESS NA MWALIMU SWAI

(PESS) PHYSICAL EDUCATION SPORTS AND SCIENCE ni kutengo cha elimu ya mazoezi ya viungo michezo na sayansi ni kitengo ambacho kinatoa waalimu wa michezo hapa Tanzania ikiwa ni pamoja na mafunzo ya aerobics na gym.


Katika picha ni wanafunzi wa mwaka wa tatu wakipata mafunzo ya ufundishaji wa mazoezi ya aerobics wakifundishwa na mwalimu Omar Swai.


Saturday, January 15, 2011

NAMNA YA KUFANYA MAZOEZI YA KUJENGA MISULI

Watu wengi wanaokwenda gym kufanya mazoezi ya kujenga misuli kwa mara ya kwanza,hudhani kwamba inachukua muda mfupi kupata misuli mikubwa.
Siyo hivyo wanavyofikiria,misuli huchukua muda kujengeka na lazima uwe mvumilivu wa maumivu ya mwili na hata pindi ufanyapo mazoezi hayo.

Pia ujue namna ya kufanya kwa wakati husika pamoja na lishe bora,nikiwa na maana ule chakula cha kutosha japo miilo minne au mitano yenye virutubisho sahihi ya kujenga mwili pamoja na mazoezi ambayo unakuwa na patna wako hapo ndipo mambo ya kujenga mwili nakupendeza huwa.

KATIKA PICHA WADAU WA KUJENGA MISULI KWENYE GYM YA REDS ILIYOPO KINONDONI WAKISIMAMIANA HUO NI MFANO MZURI KWA WADAU WENGINE.

Thursday, January 13, 2011

WAGENI KUTOKA NORWAY WAPAGAWA NA GYM YA CHUO KIKUU UDSM

Katika picha hapo chini inaonyesha mama wa kinorway profesa Birgit wa chuo kikuu cha Oslo akiwa amepagawa na mazoezi ya aerobics ya mwalimu Omar Swai chuo kikuu cha mlimani UDSM, na wadau wengine wa bongo.





Friday, January 7, 2011

WADAU WA AEROBICS CHUO KIKUU UDSM WAPAGAWA NA MAZOEZI YA MWALIMU OMAR SWAI

Katika picha hapo chini wadau wa mazoezi ya aerobics wakiwa wanajifua kwa raha zao katika gym ya Chuo kikuu mlimani udsm mazoezi yakiongozwa na mtaalam wa aerobics mwalimu Omar Swai.