Powered By Blogger

Kuna umuhimu wa kufanya mazoezi?

Tuesday, December 28, 2010

WANAFUNZI WA CHUO KIKUU UDSM WAPATA HAMASA YA KUFANYA MAZOEZIYA KUJENGA MISULI

Katika picha hapo chini inaonyesha wadau wanafunzi wa UDSM wakijifua katika mazoezi ya kujenga misuli.



Friday, December 24, 2010

RAISI WA UDSM AKIWA KWENYE GYM NA WADAU WA MAZOEZI

Hivi ndivyo wadau wa gym ya Mlimani UDSM wakifurahia mazoezi katika mashine wakiwa na raisi wa wanafunzi wa Udsm.




Thursday, December 23, 2010

CHUO KIKUU DAR ES SALAAM YAFUNGUA GYM YA KISASA YA MAZOEZI

KATIKA PICHA HAPO CHINI NI WADAU WA MAZOEZI YA AEROBICS WAKIONGOZWA NA MWALIMU OMAR SWAI AMBAE NI MTAALAMU WA MAMBO YA GYM KATIKA KITENGO CHA ELIMU YA MICHEZO NA SAYANSI(PESS)



Wednesday, December 22, 2010

MWALIMU ADAM KATIKA AEROBICS

Katika picha mwalimu Adam Gwao akiwa kwenye mazoezi ya chini Lamada Hotel




Saturday, December 4, 2010

LIKIZO YA KRISMAS NA NAMNA YA KUCHUNGA USIZIDI UZITO

Mara nyingi kipindi hiki cha mwezi wa Desemba wadau wengi wa mazoezi huwa ni wakati wa kupumzika na kukaa na familia zao, ambao kwa muda mrefu watoto wao walikuwa mashuleni.

Hata hivyo wengine ni wakati muafaka kwa wao kuchukua likizo na kusafiri kuelekea makwao.

Kwa makusudi ninazungumzia kipindi cha skukuu ya krismas ambacho mtu huenda kula bila ya mpangilio na hata kusababisha maradhi ambayo hapo awali aliweza kuyamudu kwa kufanya mazoezi.

Jambo la muhimu ni kujaribu kuchunga usirudi pale ulikotoka na kujiweka katika afya madhubuti uliyonayo hapo mwanzoni kipindi ufanyapo mazoezi.

Kuwe na umuhimu wa kujichunga na uzito ulokithiri kwa kufuata mpangilio wako wa kila siku. Yaani usizidishe chakula kupita ili kuchunga kuongezeka uzito usio na mpangilio maana baada ya siku unaanza palepale kama zamani.

Nini cha kufanya ni wewe kujaribu kutokula wanga kwa wingi na wakati wa usiku upate chakula chepesi.

Nakutakieni KRISMASI NJEMA NA AFYA NJEMA.