Powered By Blogger

Kuna umuhimu wa kufanya mazoezi?

Tuesday, November 23, 2010

WAKILI NYANGE MDAU ANAEPENDA MAZOEZI

Mara nyingi watu wanaojishughulisha na sheria huwa hawana muda wa mazoezi, lakini wakili Nyange yeye hakosi mazoezi na anajua kuyafanya na kwa bidii.

Siku hii ya leo nachukua fursa hii kumzungumzia mdau wa mazoezi Wakili Nyange, amefanya mazoezi kwa miaka mingi na anajua faida ya mazoezi,pia amehakikisha familia yake nao wanafanya mazoezi.

Kwa kweli nampongeza sana na kumfagilia na namombea aendelee na bidii yake huwa an jina lake analolipenda wakati wa mazoezi na pia ni staili inaitwa ding dong huipenda sana ambayo mimi nili
buni.


Katika picha hapo chini advocate Nyange amevaa fulana nyekundu na bukta nyeusi anafya mazoezi ya ding dong step kulia nyuma.

Sunday, November 7, 2010

WADAU WA MAZOEZI YA AEROBICS KATIKA HOTEL YA LAMADA

Mara nyigi mazoezi kama haya husaidia kuondoa matairi au mikunjo iliyopo pembeni mwa mbavu.

Hakikisha unafanya mazoezi hayo mara kwa mara husaidia kuondoa mikunjo ambayo imegeuka kuwa mafuta pembeni mwa mbavu kwa muda mfupi,ukizingatia dayati.

Katika picha hapo chini wadau wakifanya mazoezi ya (oblique) yaani kuondoa mafuta pembeni mwa mbavu.

Tuesday, November 2, 2010

KUTANA NA MDAU WA AEROBICS WA SIKU NYINGI MR MGENI

Anajulikana kwa jina la Mgeni lakini siyo mgeni wa mazoezi bali nia mdau aliyebobea katika mazoezi ya aerobics tangu enzi ya uwanja wa taifa hadi leo hii.

Katika picha hapo chini Mgeni yuko na wadau wa kike akiwapa moyo wa mazoezi kulia kwake ni zahra na kushoto erika katika club ya ok body shape iliyopo Lamada hoteli