Powered By Blogger

Kuna umuhimu wa kufanya mazoezi?

Friday, April 30, 2010

CHAKULA UNACHOTAKIWA KULA WAKATI UKITAKA KUPUNGZA UZITO

Katika maisha ya kawaida watu wengi hupenda kula nyakati za usiku, hii ni kwa sababu kwa wale ambao wanafanya kazi maofisini huwa hawapati mlo mzito wakati wa mchana.

Kutokana na sababu hiyo basi yeye hupata mlo nyakati za usiku akiwa na familia yake Ni kweli kula ni muhimu katika maisha ya binaadamu yeyote lakini wakati wa usiku huwa mwili hauhitaji virutubisho kwa kuwa hufanyi kazi yoyote inayo tumia kaloriz.

Hii hukufanya kunenepa bila ya wewe kujua unanenepeshwa na nini ukiulizwa unasema kwanza mimi nala mara moja kwa siku au mara mbili.

Kama ukiona umekosa muda wa kula mchana hebu jaribu kula matunda kwa wingi hii itakusaidia kutokula chakula kingi wakati wa usiku ule.

Kwa kawaida binaadam anatkiwa apate kalori 1500 kiwango hiki ni tosha kwa uhai wako na afya.

Thursday, April 29, 2010

NAMNA YA KUFANYA YA MPANGILIO WA KULA CHAKULA KWA WALE AMBAO WANATAKA KUPUNGUZA UZITO.

Kwa wale ambao ni mara yao ya kwanza kabisa kufanya hili zoezi la kupunguza uzito, wataona ni vigumu lakini ukizingatia haya maelezo basi wewe utafanikiwa. Jaribu kuwa unajiamini kwanza kwa kuamua kupunguza uzito uliokithiri, jaribu sana kupangilia mda wako wa kula ikiwa unakula chakula cha mchana saa 7 iwe ni kawaida yako kula mda ulopangia.

Mlo wa siku ni chai ya asubuhi ua kifungua kinywa nikiwa na maana kama upate chai ya kutosha wakati wa asubuhi.
Kwa sababu unapopata chai ya kutosha ndivo hutotamani kula hovyo hovyo bila ya mpangilio mpaka ule muda wako wa kupata chakula cha mchana.

Namna ya kujipangia miilo yako:
-Jaribu kupunguza kiasi cha chakula unachokula kila siku (ikiwa unakula sahani ilojaa unakula nusu yake).
-Punguza mafuta kwenye chakula unachotumia.
-Punguza sukari katika chai, au vitu vitamu kama keki, soda,na choklet.
-Punguza pia chumvi kwenye mlo wako yaani ile chumvi ya kuongeza mezani.
-Jaribu kuchukua muda pindi unapokula chakula nikiwa na maana utafune chakula hadi kilainike,hii inasaidia kurahisisha usagaji chakula kwa urahisi tumboni na kwa muda unaotakiwa kusambaza kwenye mwili kupitia mishipa ya damu na kupeleka mwilini.
-Mlo wa usiku jaribu kupata chakula laini na ule mapema kama saa 3 kabla ya kulala.
- Mazoezi ni muhimu wakati unafanya diety.

Friday, April 23, 2010

bonanza la aqu aerobics south beach kigamboni

Mwalimu omar swai katika bonanza la pekee nchini la Aqua Aerobics katika hoteli ya South Beach Kigamboni
washiriki wa aqua aerobics
juu na chini wakifanya stretching baada ya aqua aerobics





Tuesday, April 20, 2010

UZITO ULOZIDI KIPIMO UNAATHIRI SANA AFYA YAKO.

Kuna watu wengi ambao wanafikiri uzito ulokithiri na unene ni afya, hapa hiyo imeshakuwa ni maradhi kwako.

Binadamu anakwenda na uzito wake wa mwili kutokana na urefu wake, hivyo ni muhimu kama una uzito zaidi ya urefu wako ni bora upunguze uzito kwa kuzingatia kupunguza kula na kufanya mazoezi.

Monday, April 19, 2010

KUNYWA MAJI NI MUHIMU WAKATI WOTE

WATU WENGI HAWAPANDI KUNYWA MAJI YA KUTOSHA KILA BAADA YA MAZOEZI AU KABLA YA MAZOEZI.

NI MUHIMU KUNYWA MAJI WAKATI UNAFANYA MAZOEZI NA PINDI UMALIZAPO,HII NI MHIMU SANA KWA AJILI YA KURUDISHIA YALE MAJI MWILINI AMBAYO YALIYOTOKA PINDI UFANYAPO MAZOEZI ILI USIJEPATA TATIZO LAKUKOSA MAJI MWILINI MWAKO, MAJI YAWE BARIDI AU VUGU VUGU.

HATA KWA WALE WANAOFANYA KAZI MAOFISINI UKIWA UMEKAA JARIBU KUWA NA TABIA YA KUNYA MAJI HII ITAKUSAIDIA KUTOSIKIA UCHOVU NA KUWA MCHANGAMFU WAKATI WOTE.

KUMBUKA ZAIDI YA PASETI 60% YA MWILI WAKO NI MAJI. HII HUKUSAIDIA KUTOPATA MAUMIVU YA MISULI AU KUKAMATWA NA MISULI.

UKIWA NA TABIA YAKUNYWA MAJI YA KUTOSHA KWA SIKU JAPO LITA 1 HUTOKUWA NA TATIZO LA KUTOPATA CHOO KILA SIKU. KWA SABABU UNATAKIWA UENDE ZAIDI YA MARA MOJA HII NI KWA AFYA BORA YA MWILI WAKO.

KAMA UKIZINGATIA MAELEZO HAYA UTAEPUKA MATATIZO AMBAYO ULONAYO NAYO HIVI SASA.

Saturday, April 17, 2010

UBAYA WA KUWA NA KITAMBI

Katika maisha ya kawaida kuna watu wengi hupenda kuwa na kitambi kwa sababu eti, ukiwa na kitambi wewe ni tajiri una pesa na wengine hudhubutu kusema ni heshima ukiwa na kitambi.

Hapana hizo ni fikra potofu kabisa,kitambi siyo afya bali ni ugonjwa. Maana ukishakuwa na kitambi uwezo wa mambo fulani hupungua hata ukitembea hatua chache huwa unahema sana kama umekimbia.

Maana kwenye hicho kitambi kilichopo ndani yake ni mafuta matupu, hivyo hata moyo wako unakuwa umezingirwa na mafuta kiasi cha kutofanya kazi yake ya msukumo wa damu kwenye mwili ipasavyo kwa kuchelewa kepeleka damu kwanye mwili inabidi moyo ufanye kazi yake kwa ugumu ndipo unajikuta una tatizo la presha kupanda, ukienda kumuona daitari hukushauri kupunguza uzito au kutokula vitu vya mafuta.

Dawa yake ni kufanya mazoezi kila siku hii, itakusaidia kuondoa mafuta ambayo yamezingira moyo wako usifanye kazi yake inavyopaswa. Fanya mazoezi epuka maradhi kama haya.

Mazoezi ya asubuhi

Mazoezi ya asubuhi ni muhimu sana kwa kila mtu mwenye uwezo wa kuamka muda wa saa 12 wakati jua bado halijachomoza na kuanza kutembea au kuimbia.

Hii hukufanya uwe mchangamfu mchana kutwa kufanya kazi bila ya kusikia uchovu wa aina yoyote mwilini mwako.

Pia hata kwa wale wanaofanya sehemu za vituo vya mazoezi(gym) inakuwa ni sehemu ya salama zaidi na uhakika wa kufanya mazoezi chini ya uangalizi wa mwalimu.

Friday, April 16, 2010

mazoezi ni muhimu kila siku

Kila siku ya maisha yako kufanya mazoezi ni muhimu kwa sababu unakula pia unahitaji kupunguza yale ambayo yasiyohitajika kwenye mwili.

Kwa kufanya mazoezi na kutokwa jasho hii inasaidia kuufungua matundu yaliyomo kwenye ngozi yako.

Kwa wale ambao wanafanya mazoezi nyumbani inabidi uendeshe baiskeli au upande ngazi zenye mpandio usopungua mitatu kwa muda wa dakika 20 utakuwa umefanya mazoezi ya kutosha.

step aerobics

wanafunzi wa mlimani wakijiandaa kuanza mazoezi ya step aerobics

MAZOEZI YA AEROBICS

Mwalimu Omar Swai akiongoza darasa la
Aqua aerobics South Beach hotel, Dar es salaam

NINI MAZOEZI YA VIUNGO: KWA NINI UNAFANYA MAZOEZI?

*UMUHIMU WA KUFANYA MAZOEZI KATIKA MAISHA YAKO.
Leo nizungumzie mambo haya matatu niliyoanza nayo hapo juu.Kwa wale ambao wanafanya mazoezi kila siku na wale ambao wanafanya mara mbili au tatu kwa wiki.

Swali : Kwa nini unafanya mazoezi ?
Unafanya mazoezi kwa ajili ya afya bora ili kuepuka maradhi ya mara kwa mara ambayo pia ni rahisi kupata kwa mtu ambaye hafanyi kabisa mazoezi katika maisha yake.

Pia mazoezi yanasaidi kukufanya kuonaekana kijana mchangamfu wakati wote na pia
hukuongozea maisha.

Mazoezi husaidia moyo wako uwe madhubuti katika mapigo yake, kufungua zaidi mishipa ya damu inayopeleka na kutoa damu katika moyo.

Pia mazoezi huwezesha mapafu yako kuwa na uwezo wa kupumua bila kusikia tofauti yoyote wakati wa mazoezi na baada ya mazoezi ukiwa umepumzika.

Magojwa mengine ambayo utaepukana nayo ukiwa unafanya mazoezi ni kama vile kansa, pumu na ugonjwa wa moyo mazoezi ni dawa tosha kwa haya maradhi niliyo kujulisha hivyo usifanye ajizi anza sasa uone faida yake.

Hali kadhalika kwa wale wenye maradhi ya ukimwi mazoezi husaidia sana kurefusha maisha yao.

MAZOEZI UNAYOHITAJIKA KUYAFANYA MUDA WAKE
Yapo mazoezi ya aina nyigi yakiwapo ni pamoja na kuendesha baiskeli, kucheza mpira wa wavu, kutembea kwa mwendo wa haraka au kwenda sehemu maalum ya kufanyia mazoezi (fitness centre) na kuogelea.
Muda wa kufanya mazoezi usipungue dakika 30-60 kwa muda huu utakuwa umefanya mazoezi ya kutosha kwa siku hiyo.
Siku hizi imekuwa ni jambo la muhimu na la maana sana kufanyia mazoezi kwenye sehemu maalum (fitness centre) Huku kunakuwa na wataalam ambao wanasimamia na kufundisha aina ya mazoezi unayotakiwa kufanya yakiwemo madarasa ya aerobics na gym kunyanyua vitu vizito na kujenga mwili.

Leo tuzungumzie mazoezi ya aerobics
na unapata nini kwenye aerobics.
Kwa kufanya aerobics kila siku inakufanya uwena uwezo wa kuwa na mapigo mzuri moyo.Hukusaidia mapafukutumia hewa ya oksijen kwa uhakika na pia kudhibiti uzito wa mwili na kukufanya uwe mchangamfu kila wakati.
NINI MAZOEZI YA AEROBICS
Aerobics maana yake ni matumizi hisika ya oksijen katika mazoezi ya viungo ambayo yanaongozwa na muziki maalum kwa ajili ya mazoezi ya mwili.
Mazoezi ya aerobics yanasaidia kufanya moyo uwe uwezo madhubuti wa kusukuma damu kutoka kwenye moyo na kwenda mwilini na kurudi tena kwa mzunguko wa kawaida bila kuwa na dosari.

Mazoezi ya aerobics yanakufanya kupumzisha akili kwa kupunguza mawazo maana ukimaliza kufanya haya mazoezi hujisikia kupumzika.
Halikadhalika huondoa maumivu ya misuli yako ya mwili na huongeza uwezo wako kimwili kukufaya mtu mwenye furaha wakati wote.

MAZOEZI YA AEROBICS NI KWA AJILI YA NINI
Mazoezi ya aerobics ni kwa ajili kila mtu bila kujali jiinsia au umri hii ni kwa ajili ya watu wote ambao wameamua kufanya mazoezi ya mwili kwa ajili ya afya zao.

Baada ya utafiti wangu wa takriban miaka kumi katika mazoezi ya aerobics, darasa la aerobics lilikuwa likihudhuriwa na idadi kubwa ya wanawake kuliko wanaume hii ilikuwa ni fikra potefu walizokuwa nazo wanaume kwamba mazoezi ya aerobics ni kwa ajili ya wanawake tu.

Lakini kuanzia mwaka wa 2000 kumekuwa na mabadiliko kwa wanaume wengi kujiunga na mzoezi ya aerobics hivi sasa kuna mwamko mkubwa kwa wanaume kufanya haya mazoezi. Katika kufanya mazoezi aerobics inaupa mwili uwezo wa kupitisha hewa ya oksijen kwa urahisi zaidi na uhakika na pia kuupa moya uwezo wa kupiga mapigo yake kwa dakika wakati unapofanya mazoezi.

Mazoezi ya aerobics ni lazima yafanyike japo kwa muda wa dakika 30-60 na iwe ni mara 3 au 5 kwa wiki kwa ajili ya kuufanya mwili kuwa mchangamfu kwa wakati wote na kupunguza mafuta na uzito uliokithiri.


MAZOEZI YA AEROBICS NA MOYO
Hewa ya oksijen ni muhimu sana mwilini kwa ajili ya kuruhusu kemikali kupelekwa kwenye mwili.

Moyo umetengenezwa kwa misuli ambayo husukuma hewa ya oksijen na damu kwenye mwili wote.

Mazoezi ya aerobics huzidisha uwezo wa mapafu kuyapa oksijen na kuipa nguvu misuli ya moyo na kuwa na uhakika wa kuaminika kwa kusukuma oksijen na pia husaidia kuondoa maradhi ya moyo.

Binadamu wa kawaida ambaye hafanyi mazoezi mapigo yake ya moyo ni mara 75 kwa dakika lakini kwa wale wafanyao mazoezi kila siku mapigo ya moyo wao huwa mara 55 kwa dakika.

MAZOEZI YA AEROBICS YANAVYOSAIDIA KUTOONGEZEKA UZITO WA MWILI
Mtu huongezeka uzito pindi anapokula bila mpangilio (kula hovyo) kula chakula kwa wingi bila kupanga wakati wa kula na kula milo zaidi ya mitatu bila kufanya mazoezi.

Ni vizuri kupata lishe bora ambayo haina mafuta sana na mazoezi kwa ajili ya kupunguza uzito kwa uhakika zaidi ya mlo wako wa siku pata chai ya kutosha asubuhi mchana pata chakula kama ulikuwa unakula sahani ya chakula iliyojaa kula nusu sahani na usiku pata chakula chepesi kwani nyakati za usiku mwili hauhitaji tena virutubisho vya aina yoyote ile hadi kesho yake.

NAMNA YA KUEPUKA KULA BILA MPANGILIO
Kuna njia nyingi ambazo zitakufanya ubadilishe tabia ya kula bila mpangilio lakini njia bora ya kufuatia ni kuanza kupunguza kula vitu vya sukari polepole na hii ni baada ya wiki kadhaa utakuwa umezoea na hutorudia tena mazoea hayo kumbuka nikizungumzia vitu vya sukari ni kama vile chocolate, soda, keki
Unaweza kula vitu kama matunda ambayo yana sukari ya kutosha.
Pia jaribu kuepuka kula nyama nyekundu nikiwa na maana nyama ya ng’ombe na mbuzi, bali utumie nyama ya kuku na samaki.
Kumbuka unavyofanya mazoezi ndio utakavyokula vizuri bila kuogopa utaongezeka uzito



KARIBU KATIKA DARASA LA MAZEOZI YA VIUNGO

NAITWA OMAR SWAI. NI MWALIMU WA MAZOEZI YA VIUNGO. NACHUKUA NAFASI HII KUWAKARIBISHA KWENYE BLOG HII AMBAYO ITAKUWA INAZUNGUMZIA MAZOEZI YA VIUNGO, WANA MAZOEZI NA SEHEMU ZA MAZOEZI PAMOJA NA LISHE
KARIBU SANA. UNAKARIBISHWA KUTOA MAONI PIA NA KUULIZA MASWALI.